Jana tarehe 09/08/2017 Action Aid wamefanya kikao chao cha Tathmini ya Kazi walizofanywa kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Januari-2014 hadi Januari 2017
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Caritas uliopo Kilindoni Mafia kuanzia saa 08.30 -10.30 kiliwashirikisha waadau mbalimbali wakiwemo:-
a) Wakuu wa idara tisa na kitengo kimoja kutoka Halmashauri ya Wilaya(Mipango, Maendeleo ya Jamii, Mifugo na Uvuvi, Kilimo na Ushirika, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Idara ya Mazingira, Idara ya Uthibiti ubora wa Elimu na Vitengo vya TEHAMA na Sheria)
b)Maafisa watendaji wa vijiji
c) Maafisa watendaji kata
d)Wenye viti wa vijiji
e)Viongozi wa dini
f)Watu/viongozi mashuhuri
g)Walimu , wanafunzi , wazazi na kamati za shule
h)Ushirika wa wavuvi
i)Wawezeshaji maendeleo ya jamii (CDFs)
j)Watoa taarifa toka katika Jamii(CRPs)
k)Vikundi vya haki za wanawake
l)Timu za ufuatiliaji wa mfumo wa matumizi ya umma (PETs) na
m)Polisi – dawati la jinsia
Kazi zilizofanyika ni hizi zifuatazo:
a) Kampeni ya kupinga mimba za utotoni.
b)Masuala ya utetezi juu ya haki za watoto
c)Mpango wa ufadhili kwa mtoto (namna ya kuandika barua za kuomba ufadhili)
d)Kuelimisha umma juu kodi na uwajibikaji wa umma.
e)Kuhakikisha Usalama wa chakula (Uvuvi)
f) Kutoa elimu juu ya Haki za wanawake na watoto na
g) Kutoa ufadhili katika huduma za kijamii( Elimu na Afya)
Kwa taarifa ya kina soma kiambatanisho hiki
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.