Maazimisho ya kilele cha nanenane mwaka 2017 yalifanyika kiwilaya yalifanyika katika kata ya Baleni, kijiji cha Baleni katika viwanja vya ofisi ya Kata Baleni.
Mgeni rasmi katika maazimisho hayo alikuwa Katibu Tawala Wilaya Bw. Gilbert Sandagila kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya.
Katika maadhimisho walihudhuria watu mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mafia Mh. Mbaraka Dau, Kaimu Mkurugenzi Wilaya Bw. Emmanuel Skainda, wakuu wa idara mbalimbali za serikali na asasi zisizo za kiserikali, viongozi wa dini na vyama mbalimbali vya siasa, viongozi ngazi ya kata na vijiji wa Mafia na wananchi mbalimbali .
Katika maazimisho hayo mgeni aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho yakiwemo ya ufugaji bora wa ng'ombe, kilimo cha mbogamboga na matunda, kilimo cha mpunga, usindikaji wa vyakula (mbogamboga mboga na matunda) , uzalishaji wa maziwa na samli pamoja utengenezaji bidhaa mbalimbali linalotokana na zao la mwani.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.