Madiwani wa Halmashauri wajengewa uwezo juu ya mpango wa ukuzaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni Wah. madiwani, wakuu wa Idara na vitengo vya Halmashauri.Kaimu Afisa Elimu msingi aliwasilisha Taarifa fupi kuhusu Elimu kwa ujumla na mpango wa LANES ambapo alisema Mafia kuna jumla ya shule za msingi 34 ambapo kati ya hizo, 32 ni za Serikali na 2 ni za mashirika ya Dini. Katika kipindi cha kati ya mwaka 2012 - 2016 wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza walikuwa ni 100% ya wanafunzi wote waliofaulu.Afisa Elimu ya watu wazima ndugu Amjadi O. Sadallah aliwasilisha mada juu ya LANES na malengo yake ambapo alisema kuwa katika utekelezaji wa mpango huu, serikali imewapatia mafunzo walimu wa Memkwa Maalum 15, walimu wa Elimu maalum 2, walimu wanaofundisha madarasa ya KKK 170,waratibu Elimu kata 8 na kamati za shule za serikali 32. Kwa sasa vituo vya kutolea Elimu ya MEMKWA MAALUM vipo 8 ambavyo ni: Shule ya msingi Bweni, Kanga, Jimbo, Kifinge, Kungwi, Kigamboni, Kilindoni na Kiegeani. Mwisho aliwaomba wah. madiwani kusaidia katika kuwatambua na kuhimiza wale wote wasiojua KKK kuhudhuria katika madarasa ili waweze kupata stadi hizo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.