Naibu Waziri wa Maji Mh. Jumaa Hamidu Aweso,alifanya ziara Wilayani Mafia mnamo tarehe 18/10/2017 . Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua miradi ya maji na miundombinu iliyopo.
Alipata fursa ya kutembelea vyanzo kadhaa vya maji ikiwemo miundombinu ya maji iliyopo ktk mamlaka ya maji ya mji mdogo Kilindoni , ambapo aliona uchakavu wa miundombinu hiyo alisema serikali itatoa Tsh. Milioni 39 kwa ajili ya kuboresha miundombinu hiyo.
Alitembelea pia Kisiwa cha Jibondo ambapo alikagua Marambo 3 ya maji, mradi wa kubadili maji chumvi kuwa maji baridi na mradi wa maji ambao chanzo chake kipo kijiji cha Kiegeani eneo la Kipama (Mradi huu bado haujakamilika). Alipata pia fursa ya kuzungumza na wananchi wa Jibondo na aliahidi kutatua kero ya maji kisiwani hapo na alimuagiza Mbunge wa Mafia Mh Mbarak Dau kufuatana na Mkandarasi wa maji Mafia kwenda Wizara ya maji kuhakikisha usanifu wa mradi wa maji Jibondo unakamilika na kupata kibali kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.