Mkurugenzi Mtendaji (W) , Bw. Erick C. Mapunda amefanya kikao na wananchi wa eneo la Kitomondo kata ya Kiegeani na wananchi walinunua viwanja lakini bado hawajaonyeshwa viwanja vyao. Mkurugenzi alisema kuwa tayari Halmashauri imeshapima viwanja eneo la ulanzini na tayari vimeshatengenezewa hati za umiliki hivyo wajitokeze kwa wingi kuvinunua. Pia aliendelea kufafanua kuwa fedha itakayopatikana itatumika kulipa fipa fidia ya ardhi iliyochukuliwa na kupimwa viwanja na hatimaye waliolipiwa wataonyeshwa viwanja vyao.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.