KWA MAENDELEO ENDELEVU YA WATU NA TAIFA NI LAZIMA TUTUMIE TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
Kupitia kauli mbiu mama ya Mwenge maalum wa Uhuru kwa mwaka 2021 isemayo "TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, itumie kwa usahihi na uwajibikaji" Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi ameitaka jamii kutambua matumizi sahihi ya TEHAMA ili kupata Maendeleo endelevu katika Jamii na Taifa kwa ujumla.
"Tunasisitizwa haya kutokana na wimbi kubwa la wizi wa kimtandao, uchochezi, kusambaa kwa habari za uongo, lakini pia mmomonyoko wa maadili hasa kwa Vijana. Kwa hiyo tunaendelea kusisitizwa na Mbio za Mwenge wetu wa Uhuru kutumia teknolojia hii kwa usahihi ili kuleta maendeleo."
Mwenge huo pia ulitembea kuzungukia miradi umbali wa kilometa 77.8 ambapo Pia mjasiriamali ndugu Rajabu Kambi Amanzi alitembelewa na Mwenge na kuona uendeshaji wa biashara ya utengenezaji wa fenicha.
pia MWENGE ulizindua mradi wa Shamba la mikorosho lenye ukubwa ekari 60 linalomilikiwa na ndugu Abdallah Said Kijambia pamoja na trekta
Aidha , mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Kilimahewailimahewa wenye thamani ya Tshs. 61.2 m ikiwa serikali 60m na mchango wa jamii 1,200,000 uliwekewa jiwe la Msingi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.