Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia idara ya usimamizi na uratibu wa maafa imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kibinadamu kwa wananchi wa wilaya ya Mafia waliopata madhara ya mvua kubwa iliyonyesha mfululizo kwa siku 14 ( kumi nne). Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na magodoro 95, mablanketi 120, ndoo za maji zenye ujazo wa lita ishirini 50, ndoo zenye ujazo wa lita kumi 100 na madumu yenye ujazo wa lita kumi 50. Msaada huo ulipokelewa na mh. Mkuu wa Wilaya Shaib Nnunduma na kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji (W) ili kuwafikishia walengwa.
Jumla ya kaya 59 zilipatwa na madhara mbalimbali yakiwemo kubomokewa na nyumba, makazi kuzingirwa na maji ndani na nje pamoja sehemu mbalimbali za nyumba kupata nyufa. Madhara hayo yalitokea kwa kiwango kikubwa katika kata za Kilindoni (kaya 08 ), Kiegeani (kaya 30), Ndagoni (kaya 02 ) na Kirongwe (kaya 19).
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mafia mh. Shaib Ahmed Nnuduma ameishukuru ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutoa msaada kwa wananchi waliopata madhara hayo huku akitoa rai taasisi na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kuendelea kutoa misaada mbalimbali kwa kaya hizo kwani nyingi hazina makazi na kwa .sasa wengi wao wamesitiriwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo lilianza tarehe 03 Mei, 2021 na kukamilika tarehe 05 Mei, 2021 ambapo jumla ya kaya 80 za kata za (Kilindoni kaya 14, Kiegeani 34, Ndagoni kaya 02, na Kirongwe kaya 30) zimenufaika na msaada huo huku zikushukuru kwa msaada huo kutoka serikalini.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.