Shirika la ActionAid lilifanya mikutano miwili katika ngazi ya jamii yenye lengo la kushirikisha jamii katika kutathimini shughuli zilizo tekelezwa na shirika kwa kipindi cha miaka mitatu (2015/2018), pamoja na kupokea mapendekezo ya mpango mkakati mpya utakao tekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2018/2021. Tarafa ya kaskazini mkutano ulifanyika katika ofisi ya Kata ya Kirongwe na Tarafa ya kusini katika Ofisi ya kata ya Kiegeani.
Mikutano hiyo ilishirikisha wajumbe mbalimbali kutoka katika vijiji vya tarafa ya kaskazini na kusini pia, wajumbe hao walikuwa ni Watendaji kata ya Kirongwe na Kiegeani, wenyeviti wa vijiji, watendaji, wenyeviti wa kamati za shule, walimu, wanafunzi, wawakilishi wa baraza la haki za watoto na wanawake, CDF,YPC, Wavuvi na viongozi wa dini.Jumla ya watu 120 walishiriki.
Katika kipengele cha mapitio ya mpango mkakati wa 2015/18, Wajumbe walipata fursa ya kujadili shughuli zilizotekelezwa na shirika, Mafanikio, changamoto na mafunzo yaliyopatikana kupitia kazi hizo
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPATAARIFA YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO MKAKATI WA AATZ MAFIA KWA MWAKA 2015(2).docx
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.