Wageni kutoka nchi ya Misri Eng. Ahmed Mounir na Eng. Yasser Abbas waliwasili kisiwani Mafia mnamo tarehe 27/07/2017 lengo lao kubwa lilikuwa kutafuta eneo la kuwekeza.
Baada ya kuwasili kisiwani Mafia walienda kusaini kwenye kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa Wilaya na kusomewa taarifa fupi ya kisiwa cha Mafia na baada kupelekwa kwenye maeneo mbalimbali yanayofaa kwa uwekezaji.
Baadhi ya maeneo yaliyotembelewa ni :-
1. Fukwe ya Bahari ya Kanga maarufu kama kwa Mwinyi masunda
2. Fukwe ya Bahari iliyopo kijiji cha Banja
3. Mkondo wa Bahari ujulikanao kama "tembo nyama" uliopo kijiji cha Banja. Hili eneo ambalo bahari ikijaa na lenyewe hujaa maji na maji yakitoka eneo hili huwabaki mchanga na kutumika kama fukwe ambapo wananchi na watalii mbalimbali huenda kupumzika.
Baada ya ziara ya maeneo hayo wageni wawekezaji waliondoka kuelekea mbuga za wanyama Selous na kuahidi kutoa ripoti yao mapema baada ya kukamilisha ziara zao katika maeneo mbalimbali nchini.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.