Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imeadhimisha kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima leo tarehe 7 Septemba 2023 na kuhudhuriwa na wakuu wa idara mbalimbali, viongozi wa siasa na taasisi, viongozi wa kata na kijiji, walimu na wananchi.
Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Kauli mbiu isemayo " Kukuza uwezo wa Kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika; Kujenga misingi ya Jamii endelevu na yenye amani" yamefanyika katika eneo la Miembe Mitatu lililopo kata ya Kilindoni.
Pamoja na maadhimisho hayo, jamii ilipata fursa ya elimu kuhusu shughuli za ujasiriamali kutoka Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, makundi ya wajasiriamali na benki ya NMB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Mwl. Kassim Ndumbo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, ameitaka jamii kutumia fursa zilizopo za ujasiriamali kujiendeleza kiuchumi ili kuweza kusomesha watoto.
Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima nchini hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe moja hadi tarehe tisa Septemba tangu yalipoasisiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) mwaka 1966 na kuanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1967 chini ya Uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.