Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndg. Mussa Kitungi ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji ya TEHAMA kwa Robo ya Tatu na ya Nne 2023/2024.
Kikao hicho ni kimejadili masuala mbalimbali yahusuyo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kuweka mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma, na kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi wa umma na wananchi ambapo, wajumbe walijadili mambo mbalimbali ya kuboresha hali ya usalama kwa vifaa na mifumo ya TEHAMA iliyopo Halmashauri.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao, aliwataka wajumbe kwenda kutekeleza maagizo na kuzingatia yote waliyokubaliana katika kikao hicho
Zaidi ya asilimia 85 ya mifumo ya TEHAMA imeanza kutumika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia na kusaidia utendaji kazi katika Idara na Vitengo mbalimbali.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.