Wanawake wilayani Mafia, leo Machi 06, 2025 wamefanya kongamano lililowakutanisha kutoka taasisi mbalimbali za Serikali , zisizo za kiserikali na katika jamii ikiwa ni siku moja kabla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo, ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi pamoja na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu 2025.
Aidha, amewataka wanawake wilayani Mafia kushirikiana hasa katika masuala ya kiuchumi kwa kuungana mkono.
" Tusaidiane, kama mwanamke ana biashara yoyote, sisi wanawake inabidi tuwe wa kwanza kwenda kumuunga mkono kwenye biashara yake. Maana kama lilivyo lengo la leo, ni kukumbushana na kuinuana kifikra, kiuchumi na kijamii na kupeana mikakati ya jinsi ya kuvuka salama" alieleza Mhe. Mangosongo.
Pamoja na mambo mengi ya msingi aliyosisitiza, amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia kwenye familia na jamii kwa ujumla na kusimamia malezi ya watoto na kuwapa elimu bora ili waje kunufaisha Taifa.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa mwaka huu ni " Wanawake na Wasichana 2025 Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji"
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.