Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, imetoa mafunzo kwa madiwani kuhusu usimamizi na utoaji wa Mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Mafunzo hayo yaliyolenga kuongeza uelewa kwa madiwani kuhusu utoaji wa mikopo kufuatia maboresho ya mwongozo wa utoaji mikopo ya asilimia 10, yamefanyika tarehe 09 Oktoba,2024
Halmashauri inatarajia kutoa mikopo yenye jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni 535.9 kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu; ambapo taratibu za uombaji wa mikopo zimeanza na zinatarajiwa kumalizika ifikapo Oktoba 26, 2024.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.