Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi ameongoza kikao cha kujadili kampeni ya kitaifa ya chanjo na utambuzi wa mifugo ambayo itasimamiwa na Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Kampeni hiyo inayolenga kudhibiti milipuko ya ugonjwa wa homa ya mapafu ya ng'ombe, sotoka ya mbuzi na kondoo pamoja na mdondo wa kuku inatarajiwa kuhusisha watendaji wa kata, vijiji pamoja na wataalam wa mifugo.
Ndugu Kitungi amewataka wataalam kushirikiana vyema ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa wakati na usahihi ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya mifugo yenye ubora na salama kwa walaji.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.