Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo ametoa maagizo kwa Katibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha kuwa maonesho ya Biashara na Uwekezaji yanakuwa maonesho ya kitaifa kwa Wizara kushirikiana na mkoa wa Pwani kuandaa maonesho hayo kila mwaka.
Dkt. Jafo ametoa maagizo hayo leo Desemba 17, 2024 wakati akifungua maonesho ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Aidha, ametoa rai kwa Watanzania kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini ili kusaidia kukuza sekta ya uwekezaji, pamoja na kuzitaka taasisi zinazojihusisha na masuala ya biashara na uwekezaji kuhakikisha zinaweka jitihada kwa kuwa wawezeshaji badala ya kukwamisha.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ameeleza kuwa mkoa unatarajia kuongeza viwanda kwa asilimia 30 ili kuendelea kuchangia kukuza zaidi sekta ya uwekezaji nchini.
Mkoa wa Pwani una jumla ya viwanda 1533, ambapo zaidi ya viwanda vipya 131 vimejengwa kwa kipindi cha miaka minne.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.