Meli kubwa ya Kitalii yenye jumla ya watu 442 imewasili wilayani Mafia leo Machi 26 ikitokea Moroni, Visiwa vya Comoro. Meli hiyo ijulikanayo kama "The World " yenye wahudumu wapatao 288 ( crew) na abiria 154 imefika katika eneo la Ras Kisimani Mafia ambapo watalii waliweza kupata burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na kujionea mandhari nzuri.
Akizungumza wakati wa kuwapokea watalii hao, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo, amedhihirisha kufurahishwa kwake pamoja na kutambua juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza Tanzania.
" Haya ni matokeo ya Royal Tour pamoja na Mafia Island Festival. Sisi kama Mafia tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuweza kutufungulia njia na sisi tunaanzaia pale alipoishia yeye" alisema Mhe. Mangosongo.
Aidha, amesisitiza kuwa kisiwa cha Mafia ni salama na miundombinu yake imeimarika ikiashiria utayari wake wa kupokea watalii na wawekezaji.
" Ni mara yangu ya kwanza kufika Mafia na nimeshangazwa na uzuri wake. Kila mtu amefurahi sana hasa mimi ambapo nimeweza kuona tamaduni za watu wa hapa" alisema hayo Alma Martinez, Mhudumu wa meli hiyo, raia wa Mexico
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.