Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Ndugu Shabani Shabani amewataka watumishi wilayani Mafia kusimamia taaluma zao kwa kujituma pamoja na kuwa waadilifu.
Akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika Julai 24, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri, Ndugu Shabani ameeleza kuwa ni muhimu kwa watumishi kuzipenda taaluma zao, kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya taaluma zao pamoja na kuwa tayari kuwatumikia wananchi bila malalamiko.
" Utumishi wa Umma si ajira peke yake, ni wito, isije ikatokea DHRO ( Mkuu wa Idara ya Utawala) anakutafuta saa mbili usiku kwa jambo la kiutumishi la dharura; unamwambia huwezi kutekeleza kwakuwa si muda wa kazi, hiyo si sawa, tunatakiwa tuwe 'flexible ' na hiyo ndo maana ya kuwa kazi zetu ni wito" alieleza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi ametoa wito kwa Wakuu wa Idara na Vitengo kuwatia moyo wasaidizi wao kwa kuwapa motisha bila kusahau kuwashauri namna nzuri ya kufanya kazi pindi wanapokosea kabla ya kuwachukulia hatua.
Aidha, amsisitiza watumishi kuwa waadilifu muda wote wawapo kazini ikozingatiwa kuwa utumishi wao ni kwa ajili ya wananchi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.