Vikundi 15 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu vimekabidhiwa hundi ya thamani ya Shilingi Milioni 174.7 ambazo ni fedha zinazotolewa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akikabidhi hundi hiyo leo Novemba 13, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Ndugu Rajabu Gundumu amesisitiza kuwa fedha hizo zinazotolewa si ruzuku na badala yake zinatakiwa kutumika kwa lengo lililokusudiwa na kurejeshwa kwa wakati ili wananchi wengine waweze kunufaika nazo.


Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Bi. Asha Itelewe ameeleza kuwa katika dirisha hili la tatu 2025/2026, wanufaika wa mikopo hiyo ni vikundi vinane vya wanawake, vikundi vitano vya vijana pamoja na watu wawili wenye ulemavu.
Bi. Itelewe ameeleza kuwa ni muhimu kwa wanufaika kuzingatia mafunzo waliyopatiwa katika kufanya shughuli zao za kuwaingizia kipato ili waweze kunufaika kiuchumi pamoja na kurejesha kwa uaminifu.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.