Serikali imechangia mafanikio makubwa katika sekta ya Afya wilayani Mafia kutokana na utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na ongezeko la watumishi katika sekta hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025 na miaka mitatu ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo vinne mwaka 2021 mpaka kutokuwa na vifo kwa mwaka 2024, kupungua kwa vifo vya watoto wachanga kutoka vifo 19 mwaka 2021 hadi vifo 6 mwaka 2024, ni miongoni mwa hatua nzuri katika sekta ya Afya wilayani Mafia.
" Tumepiga hatua kubwa kwenye suala la afya, tunatamani sana vifo vya watoto wachanga visiwepo kabisa " alisema Mhe. Mangosongo.
Ongozeko la vituo vya kutolea huduma za afya ni miongoni mwa maendeleo yaliyochangia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Afya, jumla ya vituo vitano vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 20 mwaka 2021 hadi kufikia vituo 25 mwaka huu, 2024, ambapo vijiji vya Kifinge, Gonge, Kiegeani, Micheni na Kilindoni vimenufaika na mafanikio hayo kwa kipindi cha karibuni.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.