Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa tanzania kupitia wizara ya Afya na TAMISEMI imeandaa Kampeni maalum ya ugawaji wa vyandarua kwa wananchi ambayo itafikia kila kaya bila malipo ikiwa ni mpango wa Serikali wa kutokomeza Malaria nchini.
Akizungumza wakati wa kikao kazi cha maandalizi ya kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya Mafia Mhe. Aziza mangosongo ameeleza kuwa zaidi ya vyandarua 41,000 vitasambazwa kwenye kaya Wilayani huku akiwaelekeza wasimamizi wa kampeni hiyo kuhamasisha wananchi kujiandikisha ili wapatiwe vyandurua vya kujikinga na kutokomeza malaria hadi ifikapo mwaka 2030.
" Napenda kusisitiza kwamba muwahamasishe wananchi kujiandikisha ili waweze kupata vyandarua na hatimaye tutokomeze malaria ili kufikia lengo la "zero Malaria" ifikapo 2030 alieleza Mhe. Mangosongo.
Akisisitiza umuhimu wa viongozi na wananchi kushiriki kampeni hiyo, mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Ndugu January Bonaventure ameeleza kuwa ni vyema kusimamia ipasavyo kampeni ili thamani ya kazi inayofanywa na Serikali imfikie kila mmoja.
Jitihada za kutokomeza ugonjwa wa malaria zimesaidia kwa kuwango kikubwa kupunguza malaria ambapo kiwango cha malaria kwa nchi ni asilimia 8.1 ikilinganishwa na asilimia 14.8 ya mwaka 2022.
"ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI CHUKUA HATUA KUITOKOMEZA"
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.