MIRADI INAYOTEKELEZWA NA HALMASHAURI.
Mradi wa ujenzi wa soko hilo unaotekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ulitengewa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.
Kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024, kiasi cha Shilingi Milioni 124.9 kimetengwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi.
Soko kuu la Kilindoni litakuwa na upekee wa aina yake kutokana na sababu zifuatazo:
- Linafikika vizuri kutokana na uwepo wa barabara.
-Lipo karibu na uwanja wa ndege wa Wilaya pamoja na bandari.
-Lipo karibu na huduma za kifedha ( Uwepo wa benki) pamoja na :Ukaribu wake na ofisi za Wilaya na Halmashauri.
Mradi unatarajiwa kukamilika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2025 ambapo jumla ya Shilingi Milioni 737.7 zinahitajika kukamilisha mradi huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kupitia Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ipo tayari kutumikia wananchi kwa kuhakikisha kuwa huduma za msingi katika jamii zinapatikana
Mradi wa Jengo la Mama na Mtoto (Hospitali ya Wilaya)
Mradi unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu (Milioni 250) na wadau wa Kuimarisha Huduma za Uzazi na Afya ya Mtoto (Milioni270) ambapo jumla ya gharama zote za mradi ni Shilingi Milioni 520.
Mradi wa nyumba za walimu, Bweni
Nyumba tatu za walimu katika Shule ya Msingi Bweni zinazotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.