Kwa muda mrefu, vituo vya kutoa huduma ya afya vilikuwa vikishindwa kubaini mapema tatizo la udumavu kwa watoto kutokana na kukosekana kwa vifaa vya upimaji.
Kwa kuzingatia hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kupitia Kitengo cha Lishe imeanza kushughulikia tatizo hilo kwa kuviwezesha vituo kupata vibao vya kupimia urefu kwa watoto chini ya miaka mitano.


Akikabidhi vifaa hivyo Januari 19, 2026, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amepongeza jitihada hiyo na kuwataka wasimamizi wa vituo hivyo kutunza vifaa na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, amewataka wazidi kutoa elimu kwa jamii hasa kuhusu lishe bora, pamoja na kutilia mkazo suala la unyonyeshaji kwa kufuata maelekezo ya wataalam kuhusu namna bora ya kunyonyesha watoto ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto.
Jumla ya vibao saba vya kupimia urefu kwa watoto chini ya miaka mitano vilikabidhiwa kwa baadhi ya watendaji wa kata na wafawidhi wa vituo ambapo vifaa vingine vinatarajiwa kuongezwa ili kumaliza kabisa tatizo.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.