Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi amewataka wasimamizi wa miradi kuhakikisha kwamba wanazingatia maelekezo ya Serikali na kuyatekeleza ipasavyo ili miradi ikamilike kwa wakati.
Ndugu Kitungi ameyasema hayo leo January 2, 2026 wakati wa kikao kazi na wasimamizi wa mradi, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, Chicco.


Ameeleza kuwa wasimamizi wana jukumu la kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa maagizo ya viongozi ili pamoja na kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kuleta thamani ya fedha.
" Mhakikishe miradi yote iliyoanza, inayoendelea na inayotarajiwa kuanza inakamilika kwa wakati ili tija ya Mhe. Rais ya kutuletea fedha nyingi za miradi iende kupatikana kwa wananchi kwa kupata huduma kutokana na miradi hiyo kufanya kazi" alisiaitiza.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.