Utangulizi
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia ni Miongoni mwa Wilaya tisa (9) katika Mkoa wa Pwani iliyoanzishwa mwaka 1959. Wilaya zingine ni pamoja na Bagamoyo, Kibaha Mji,Kibaha, Chalinze, Kisarawe, Mkuranga, Kibiti na Rufiji. Kijiografia Wilaya ya Mafia ni mkusanyiko wa Visiwa vinane kwenye Bahari ya Hindi km 195 kusini mwa Jiji la Dar es Salaam. Visiwa hivyo ni Mafia (kisiwa kikuu), Jibondo, Mbarakuni, Shungimbili, Nyororo, Juani, Bwejuu na Chole. Visiwa vya Mbarakuni, Shungimbili na Nyororo ni vya makazi ya muda tu ya wavuvi. Kisiwa cha mafia kinapatikana kati ya longitudi 39°E – 40°E na latitude 7.38oS.
Eneo na Mipaka
Wilaya ya Mafia ina jumla ya kilometa za mraba 972, kati ya hizo kilometa za mraba 407 ni nchi kavu na 565 ni eneo la maji ya Bahari ya Hindi. Wilaya ya Mafia imepakana na Wilaya za Mkuranga- upande wa kaskazini, Rufiji na Kilwa –upande wa Kusini Magharibi na Bahari ya Hindi- upande wa kusini Mashariki.
Eneo la Utawala
Wilaya ya Mafia ilianzishwa mwaka 1959, ina Tarafa mbili (Kaskazini na Kusini), Kata 8, Vijiji vilivyosajiliwa 23 na Vitongoji 136. Wilaya ya Mafia ina Jimbo moja la Uchaguzi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.