• Wasiliana nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mafia District Council
Mafia District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Ardhi, Mipango miji na Maliasili
      • Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
        • Kitengo cha Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi na Zima Mmoto
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango na Takwimu
    • Vitengo
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Tehama
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Huduma za jamii
      • Maadili
      • Fedha, Utawala, na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Kujua Sheria
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
      • YOUTUBE
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

USHIRIKISHWAJI WA JAMII NI NGUZO KUBWA YA UTUNZAJI WA RASILIMALI ZA BAHARI

Posted on: December 30th, 2025

Ushiriki wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa mazingira, hususan rasilimali za bahari, ni jambo muhimu linaloweza kuleta maendeleo endelevu hasa katika uchumi wa buluu ambapo viongozi katika ngazi mbalimbali wanalo jukumu kubwa la kushirikisha wananchi ili kufikia malengo yanayokusudiwa.

Kwa kuzingatia hilo, Shirika la WATONET limeandaa mradi wa Uimarishaji wa Vikundi Shirikishi vya Usimamizi wa Rasilimali za Bahari na Pwani ( BMU na VLC) ambao utatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2026 hadi 2028.

Akizindua mradi huo leo Desemba 30, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amewataka watekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanazingatia zaidi utendaji ili kuketa mabadiliko kuliko siasa ambazo zimekuwa zikitawala vikundi hivyo vilivyopo katika jamii.

" Ninatamani muende mkatao elimu ambayo itawafanya viongozi wa BMU kusimamia vizuri sana mazao ya bahari, pamoja na mapato na matumizi ili masuala ya vurugu hasa wakati wa uchaguzi wa viongozi yasitokee" alisisitiza Mhe. Mangosongo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WATONET Ndugu Liberatus Mokoki ametoa wito kwa viongozi wa Serikali, taasisi, wadau na wananchi kwa ujumla kushirikiana kwa karibu ili kukifanya kisiwa cha Mafia kuwa miongoni mwa maeneo yanayofanya vizuri katika masuala ya uhifadhi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu. Mussa Kitungi amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu utaakisi Dira ya Taifa 2050 kwa kujenga uchumi jumuishi ambapo kila mwananchi anaguswa na uchumi huo.

Aidha, ametoa wito kwa mashirika mengine na wawekezaji mbalimbali kujitokeza kuunga mkono mchango wa uchumi wa buluu maana Serikali imeweka mazingira wezeshi ili kufanikisha uwekezaji.

Viongozi mbalimbali kutoka vikundi shirikishi pamoja na wananchi wamepongeza hatua hii na kuweka wazi matarajio yao kupitia mradi huo.

" Miongoni mwa changamoto zilizotukuta ni migogoro ya mara kwa mara pamoja na uelewa mdogo juu ya uendeshaji wa BMU, ila sasa tunaenda kufufua matumaini mapya katika BMU zetu lakini tunaenda kufanya hughuki zetu kwa uelewa zaidi hasa katika kuimarisha doria na kuwa na takwimu sahihi za wadau wote wa uvuvi" alieleza Mkufunzi wa masuala ya hifadhi ( CBM) kutoka DOKICHUNDA ( Eneo la Usimamizi wa Pamoja- CFMA; Dongo, Kilindoni, Chunguruma na Ndagoni).

Mradi huo unaofadhiliwa na Blue Ventures utatekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika la WATONET, Halmashauri ya Wilaya ya Mafia pamoja na Hifadhi ya Bahari Mafia ( MIMP).

Matangazo

  • MWALIKO WA KUHUDHURIA BARAZA LA KWANZA LA MADIWANI November 29, 2025
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • WASIMAMIZI WA MIRADI WATAKIWA KUFUATA MIONGOZO YA SERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI

    January 02, 2026
  • USHIRIKISHWAJI WA JAMII NI NGUZO KUBWA YA UTUNZAJI WA RASILIMALI ZA BAHARI

    December 30, 2025
  • NAMNA JAMII INAVYOSHIRIKI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

    December 28, 2025
  • JITIHADA ZA UHIFADHI ZALETA MATUMAINI KWA WAKAZI WA JIMBO

    December 18, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA WAPEWA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE
Tazama Video zaidi

Viungo vya haraka

  • Home
  • Photo Gallery
  • FAQ
  • Tourism
  • Investment
  • MATOKEO YA STD VII 2022

Viungo vinavyohusiana

  • OR- TAMISEMI
  • OR- Menejimenti Utumishi wa Umma
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
  • Wizara ya Fedha na Mipango

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kilindoni-Bomani Street

    Anuani ya posta: 85

    Simu: 0232010199

    Simu ya mkononi:

    Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Katazo
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma namba 1
    • YOUTUBE

Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.