Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametoa wito kwa wadau mbalimbali waliopo nje na ndani ya wilaya ya Mafia kujitokeza kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya elimu.
Wito huo umetolewa leo Novemba 21, 2025 wakati akikabidhi seti ya viti na meza 42 katika shule ya sekondari ya Raphta iliyopo kata ya Kilindoni.
Mhe. Mangosongo ameipongeza taasisi ya 'Star for Life' kwa kutoa msaada huo ambao unaenda kupunguza tatizo la uhitaji wa viti na meza shuleni hapo.


" Star for Life hapa mmesaidia wanafunzi 42 ambao walitakiwa wakae chini, lakini pia mmetusaidia kama Serikali kutupunguzia mzigo wa utengenezaji wa hivi viti na meza. Tunatamani hili lisiishie hapa na tunawaomba wadau wengine waliopo nje na ndani ya Wilaya waiangalie hii sekta ya elimu" alieleza.
Aidha, amewataka wazazi kuendelea kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora kwa kufuatilia mwenendo wa masomo pamoja na kuhakikisha wanapata chakula wawapo shuleni kwa kuwachangia.

Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.