Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Rajabu Gundumu awaongoza wajumbe wa kamati ya lishe kujadili taarifa za utekelezaji katika robo ya kwanza Julai - Septemba, 2025.
Kikao hicho kilichofanyika leo Novemba 14, 2025 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kimetoa fursa kwa idara mbalimbali kuwasilisha taatifa za utekelezaji wa shughuli ya lishe kwa robo ya kwanza pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha utekelezaji wa majukumu kwa kipindi kinachofuata.


Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amewataka wataalam kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora katika shule, vituo vya kutolea huduma za afya na jamii kwa ujumla ili kuimarisha afya za watoto, hasa walio katika chini ya umri wa miaka mitano.
Aidha, amesisitiza juu ya umuhimu wa upatikanaji wa chakula shuleni ambapo amewataka maafisa lishe, watendaji wa kata na vijiji pamoja na walimu kushirikiana vyema na wazazi kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wawapo shuleni.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.