Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mafia leo Mei 15, 2025, limeridhia kuanzishwa kwa mradi wa kuongeza thamani na ubora wa zao la dagaa kwa ajili ya kuongeza usalama kwa walaji na kukuza soko kimataifa.
Mradi huo ujulikanao kama ' Dream' unaotekelezwa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani ( WWF) pamoja na WorldFish, unatarajiwa kuanza hivi karibuni katika kijiji cha Chunguruma kilichopo kata ya Ndagoni na kugharimu kiasi cha Dola za kimarekani 250,000.
Mradi wa ' Dream' utakaotumia nishati ya jua una lengo la kuongeza ufanisi katika uzalishaji, uchakataji, kuongeza thamani na kupunguza upotevu wa zao la dagaa na mnyororo wa thamani wa Mafia.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.