Shirika la @camfed limetambulisha rasmi mradi wake wa Stadi za Maisha wilayani Mafia likihusisha Wakuu wa Shule, Waratibu Elimu Kata na Walimu Walezi kwa kuwapatia mafunzo.
Mradi huo wenye lengo la kuwajenga vijana na kuwaandaa kimaadili, uwajibikaji, na kuwa na moyo wa kujitolea kulitumikia Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo uongozi, umetambulishwa kwa mafunzo ya siku mbili kuanzia Juni 27 hadi 28, 2024, katika Shule ya Sekondari Kilindoni, ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mohammed Hussein aliyefungua mafunzo hayo.
Awali Programu Meneja kutoka Shirika la CAMFED, Ndugu Latifa Sabuni amesisitiza kuwa ili Mradi uweze kutekelezwa vizuri, juhudi zinahitajika kutoka kwa Viongozi wa Serikali katika Usimamizi wa Mradi wa Elimu wa Stadi za Maisha katika Sekondari zote ili kupata tija ya Mafunzo haya kwa Vijana wilayani, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Shirika la CAMFED linatekeleza mradi huo katika Halmashauri 35 katika shule zote za Serikali kuanzia kidato cha kwanza.
Shirika la CAMFED ( Campaign for Female Education) ni Shirika lisilo la Kiserikali linalojikita katika kumsaidia mtoto wa kike ili aweze kwenda shule, kustawi na kumuandaa kuwa kiongozi mwenye maono na kuleta mabadiliko kwenye jamii.
Shirika limefanya mabadiliko kwa kuongeza wigo na kuhusisha watoto wa kiume ili waweze kunufaika na mradi huo.
Wawezeshaji wa Mradi wa CAMFED
Wakuu wa shule za serikali Mafia
Waratibu elimu kata Wilaya ya Mafia
Walimu wa malezi wataofanya kazi na mradi wa CAMFED
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.