Asasi ya Wanawake inayojishughulisha na uchakataji wa mazao ya bahari wilayani Mafia ( COWOFO), leo Mei 21, 2025 imekabidhi msaada wa sabani na nepi za watoto (pampers) kwa wazazi na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia.
Akikabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Asasi hiyo Bi. Sara Bakari ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwaunga mkono katika kusaidia wagonjwa, hasa wale wasiojiweza Hospitalini hapo pamoja na vituo vingine vya kutolea huduma ya afya.
" Tumekuja kuwafariji wagonjwa kwa kidogo tulichojaaliwa na Mweyezi Mungu, tunashukuru kwa kupokelewa vizuri na tunatoa hamasa kwa mashirika na wadau wengine wajitolee kuwasaidia wagonjwa" alieleza Bi. Bakari.
Akipokea msaada huo, Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia Bi. Fatuma Jabiri, ametoa shukrani za dhati kwa asasi hiyo kwa kusaidia wagonjwa na kuungana na kuthamini juhudi mbalimbali za wauguzi hospitalini hapo.
Aidha, ametoa wito kwa vikundi mbalimbali katika jamii kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji.
Asasi ya COWOFO ilianzishwa mwaka 2022 na inafanya kazi kwa kushirikiana na Hifadhi ya Bahari Mafia ( HIBAMA), Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani ( WWF), Shirika linalojihusisha na Uhifadhi wa Mazingira na Utunzaji wa Papa Potwe (WATONET), na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
Asasi hiyo imekuwa ikiwezeshwa na WWF kwa kujengewa uwezo wa namna ya uongezaji wa thamani wa mazao ya bahari ikiwemo mwani, samaki, na dagaa, pamoja na kupatiwa elimu ya utunzaji wa mazingira kutoka Hifadhi ya Bahari Mafia (HIBAMA).
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.