Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na inayoanza kutekelezwa wilayani Mafia ikiwa ni mwemdelezo wa ziara yake.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa ofisi ya kijiji cha Dongo, ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya Msingi Sikula iliyopo kijiji cha Dongo, ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Baleni, ujenzi wa jiko pamoja na ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari ya Kirongwe.
Akiwa katika ziara yake Septemba 22, 2025, Mhe. Mangosongo amezitaka kamati za usimamizi wa miradi kuhakikisha kuwa miradi inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati kwa kizingatia thamani ya fedha.


Ameeleza kuwa ni muhimu kamati zikatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia miongozo ya Serikali ya usimamizi wa miradi ili miradi ikamilike kwa ubora na wananchi waanze kunufaika nayo.
Aidha, amezielekeza serikali za vijiji kuweka nguvu katika kutekeleza miradi yao kwa kusimamia vizuri fedha za vijiji kukamilisha miradi, ikowemo ujenzi wa ofisi huku akiipongeza serikali ya kijiji cha Dongo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho kujenga ofisi.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Mangosongo amesisitiza mawasiliano mazuri kati ya wasimamizi wa miradi na viongozi kwa ngazi ya Halmashauri na Wilaya ili kuwezesha kutatua changamoto zozote zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.