Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo amewapokea wanamichezo walipowasili nyumbani Mafia na vikombe baada ya ushindi katika mashindano ya UMISSETA yaliyofanyika Kibaha, ambapo Mafia imekuwa bingwa katika mchezo wa mpira wa miguu na kuwa mshindi wa pili katika mpira wa mikono kwa wavulana.
Wanamichezo hao wamefanikiwa kutwaa vikombe vinne kati ya michezo saba waliyoshiriki.
Jumla ya wachezaji 11 wa michezo mbalimbali wamechaguliwa kwenye timu za mkoa.
Mhe. Mangosongo amewapongeza viongozi , walimu, wanafunzi na wazazi kwa ushindi na ushirikiano waliouonesha na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika kuboresha michezo.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.