Watumishi wilayani Mafia waaswa kujiendeleza kitaaluma pindi wawapo kazini ili waweze kuongeza ufanisi.
Wito huo umetolewa leo Januari 29, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndg. Mussa Kitungi wakati wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika kwa lengo la kusoma na kupitia rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
" Niwaombe sana, tuhakikishe tunajiendeleza, kujiendeleza kitaaluma ni muhimu sana, achilia mbali mafunzo ya muda mfupi. Usije ukawa umeingia katika utumishi wa umma na kutoka kama ulivyoingia" alisisitiza Ndg. Kitungi.
Miongoni mwa mengi yaliyojadiliwa ni pamoja na kuhakikisha stahiki za wafanyakazi zinazingatiwa na kupewa kipaumbele pamoja na kuweka mkazo kwa watumishi kuwajibika ipasavyo wawapo kazini ili waweze kuhudumia wananchi vizuri.
Akisisitiza kuhusu kudumisha upendo, Amani na mshikamano baina ya watumishi, Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Pwani, Bi. Susan Shesha ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo wilayani Mafia ni uhaba wa watumishi, hivyo Serikali inatanya kila liwezekanavyo kuleta watumishi hasa katika sekta ya afya na elimu.
Aidha, ametoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa bidii na kuwa wastahimilivu ili kuwatumikia wananchi badala ya kuwaza kuhama na kwenda kufanya kazi nje ya Mafia.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.