Wananchi wilayani Mafia washiriki futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango Aprili 07, 2024.
Futari hiyo iliyoandaliwa kwa ajili ya watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu, wazee na watoto ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa dini.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo ambaye ofisi yake iliratibu shughuli hiyo, alitumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Dkt. Mpango kwa kuwathamini wakazi wa Mafia hasa watu wa makundi maalum na kutoa zawadi ya madaftari, na kalamu kwa wanafunzi wenye ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo alipata fursa ya kutoa zawadi ya madaftari, na kalamu kwa wanafunzi wenye ulemavu.
" Nawashukuru viongozi walioandaa shughuli hii na kutupa wito, naomba Mwenyezi Mungu awajalie kheri na kuwaongoza kwa kututhamini" alisema Mbaraka Ally, mlemavu wa miguu.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.