Wanakikundi cha ' Tuelewane' kutoka kijiji cha Jimbo kilichopo kata ya Kirongwe wameanza kuona matunda ya jitihada zao za uhifadhi wa mazingira baada ya maeneo yaliyoharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali kuanza kurejea kwenye hali ya kawaida.
Kikundi hicho ambacho kilipatiwa mafunzo na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kupitia mradi wa #NORAD unaofanya uongoaji wa ardhi ya mikoko, kimepanda jumla ya mikoko 34, 450.


Pamoja na jitihada hizo za uhifadhi, wanajihusisha pia na shughuli mbalimbali za kuimarisha kipato kama vile uvuvi endelevu na shughuli mbadala ya ufugaji wa nyuki.
Elimu waliyoipata inawasaidia pia kuhamasisha wananchi wa kijiji cha Jimbo kutunza mazingira ili kuwa na rasilimali endelevu.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.