Kupitia mradi wa Ustahimilivu kwa Jamii za Pwani na Mifumo ya Ikolojia ya Misitu katika Kisiwa cha Mafia, shirika la Sea Sense linaendelea kuhamasisha ushiriki wa jamii katika utunzaji wa mazingira ambapo limeanzisha vikundi viwili vya mazingira katika maeneo ya Kifinge, Kungwi-Kibada yaliyopo kata ya Baleni.


Vikundi hivi vyenye wastani wa wanachama 25 hadi 30 kila kimoja, vimekuwa vikishiriki kikamilifu katika shughuli za kuanzisha vitalu vya miti ya misituni, ikiwemo mikongo na jamii nyingine za miti asilia.
Kupitia jitihada hizi, vikundi vimefanikiwa kuandaa jumla ya viriba 20,000 vya miche, ambapo viriba 10,000 vipo kijiji cha Kifinge na viriba 10,000 vipo Kungwi-Kibada. Shughuli hizi zimefadhiliwa na CEPF na FOS, na kuratibiwa na Shirika la Sea Sense kwa kushirikiana kwa karibu na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Hifadhi ya Bahari ya Mafia (MIMP).


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.