Mkuu wa mkoa wa Pwani mhe. Abubakar Kunenge ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Mafia kwa kufanikiwa kuongeza vyanzo vya mapato na kupata hati safi.
Rc.kunenge ameyasema hayo mapema Leo katika kikao cha kujadili hoja za CAG kilichofanyika wilayani Mafia mkoa wa Pwani.
Kunenge amesema "kama Kuna vitu ambavyo Mhe.Rais anavisisitiza sana na kama ninyi mmefanya vizuri wenzenu wajifunze kuongeza vyanzo vya mapato, vyanzo vipya na Sheria mpya hii nimuhimu sana kwasababu hii ndiyo inaipa halmashauri uwezo wa kufanya shughuli zote"
Kunenge amesisitiza kuwa kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato ndiyo kitakachoibadilisha Mafia.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.