Timu ya watoa huduma ya afya leo Machi 20, 2025 imetembelea Kijiji cha Chunguruma, kilichopo kata ya Ndagoni kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa MPOX.
Elimu iliyotolewa imelenga kujenga uelewa kuhusu ugonjwa huo kwa kutilia mkazo namna ya kujikinga ili kuepuka kuenea katika jamii.
" Kama ambavyo tunafahamu, eneo hili lipo kwa ajili ya kibiashara hasa ya mazao ya bahari na linakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali wa ndani na nje ya nchi yetu, hivyo tumeona ni muhimu kutoa elimu na kuongeza hamasa ya mawasiliano kutoka ngazi ya jamii kuja Idara ya Afya ili tuweze kujikinga dhidi ya ugonjwa wa MPOX" alieleza Ndugu Othman Masanga, Afisa Afya wa Wilaya ambaye pia alimuwakilisha Mganga Mkuu wa Wilaya.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.