Jamii imetakiwa kuzingatia umuhimu wa lishe bora kwa kuzingatia ulaji wa makundi matano ya chakula kwa watoto kuanzia umri wa miezi sita na zaidi ili kuimarisha ukuaji wao na kuepuka magonjwa mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa yaliyofanyika leo Oktoba 29, 2024 katika Hospitali ya Wilaya.
Mhe. Mangosongo amesisitiza kwamba wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wanapata lishe bora hasa wawapo katika hatua za ukuaji ili kuwajenga kiakili.
Ameongeza kuwa, mama mjamzito pia ana wajibu wa kuhakikisha anapata leshe bora kwa ajili ya mtoto aliye tumboni na kwa ajili yake mwenyewe.
" Tunavyopewa taratibu za kufanya kuhusu uzazi, hasa tukiwa wajawazito na baada ya kujifungua, ni muhimu kuzingatia na kufuata ushauri wa daktari na tusiishi kwa mazoea" alisema Nasra Hamisi, mkazi wa Kilindoni.
Lengo kuu la maadhimisho haya kwa mwaka huu ni kuijengea jamii uelewa wa masuala ya Lishe kwa kutoa elimu sahihi ya ulaji kwa kuzingatia Mwongozo wa Kitaifa wa Chakula na Ulaji, yaliyoongozwa na kauli mbiu "Mchongo ni Afya Yako, Zingatia Unachokula".
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.