Katika ziara iliyofanyika siku ya tarehe 09/11/2022 , wajumbe wa kamati ya fedha , mipango na utawala walitembea miradi mbalimbali ikiwemo:-
Mradi wa jengo la ofisi la Halmashauri kamati iliridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la ofisi japokuwa kuna changamoto ya uchelewaji wa mapokezi ya fedha hivyo wameshauri utafutwe muarobaini wa kutatua tatizo hili na kuhusu kuisha kwa mkataba mkandarasi mshauri wameagiza taratibu zifuatwe na aongozwe mkataba uongozwe ili aweze kukamilisha kazi yake na wameshauri fedha za ukamilishaji wa uwekaji wa umeme, mandhari ya nje ya jengo (land scaping) , samani za ofisi , uzio viombewe fedha mapema ili isichukue muda mrefu kuhamia pindi litakapokabidhiwa
Ujenzi wa zahanati kijiji cha Chemchem
Kamati imemuagiza mhandisi amsimamie fundi vizuri na kwa ukaribu ili mradi ukamilike kwa wakati , Kamati ilihiji kuhusu ujenzi wa ambapo mhandisi ujenzi aliiambia kamati kuwa fedha za ujenzi wa choo zilishatengwa taratibu za manunuzi zinaendelea
Mradi wa Uchakataji wa taka mbichi za majumbani kuwa mbolea shambakilole - Utende
Kamati ilimpongeza mmiliki wa hoteli ya shambakilole kwa ubunifu wa kuanzisha mradi wa kubadili taka mbichi kuwa mbolea, taka hizi ni za majumbani , alionesha kamati pamoja na wataalam jinsi ya kuzibadilisha taka hizo ambazo ni tishio kwa sasa na kuwa mbolea isiyo na sumu. Alisema taka hizo zinapitia hatua nne kila na kila hatua inachukua siku 07 mpaka 10 . Pia alieleza njia ya pili ya kuteketeza ama kuzibadili taka mbichi hizo ni kwa kutumia inzi maalumu wanaokula taka mbichi na baadae kinyesi inzi na inzi wenyewe wanakua mbolea hao mwisho kamati iliridhia mradi uanze.
Kuwatembelea wanafunzi walio kwenye maandalizi ya kidato cha nne katika shule ya sekondari kitomondo, wajumbe waliwapa nasaha na kuwaombea waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne , Hata hivyo kamati inayowasimamia vijana hao waliuomba uongozi wa Halmashauri kuwalipa kiasi kilichobaki katika mchango wake kwa vijana ambapo
malipo yamechelewa pia shukrani zao za dhati kwa mdau Kalamu Education Foundation (KEF) kwani wamekua mstari wa mbele kutoa msaada mkubwa hasa kwa upande wa elimu
Ujenzi wa shule mpya ya msingi Kigamboni
mbao haziko treated, na zinabaki nyingine zina
kamati ilishauri kamati za ujenzi kabla hazijafanya manunuzi zipeleke mahitaji kwa mhanandisi ili aweze kushauri , pia walishauri mbao zitakazobakia zilipelekwe sehemu zenye miradi inayoondelea kuepusha uharibifu na kupata / kuongezea mahitaji yaliyopungua
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.