Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, leo Februari 01, 2025 imetembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya sekondari Jimbo katika kata ya Kirongwe, ujenzi wa zahanati ya Kibada katika kata ya Baleni, ujenzi wa shule ya msingi Sharaza iliyopo kata ya Kirongwe, eneo lenye ukubwa wa hekari 56 la shamba la mkulima katika kata ya Ndagoni, pamoja na ukaguzi wa mwalo uliopo Tumbuju.
Kamati imesisitiza ukamilishaji wa miradi kwa wakati ili wananchi wasikae muda mrefu bila kupata huduma pamoja na kuwataka wasimamizi wa miradi kufanya kazi kwa ushirikiano na uaminifu.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.