Kamati ya lishe ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Ndugu Mussa Kitungi ikijadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya nne (Aprili - Juni) ya mwaka 2024/2025, hali ya utoaji wa chakula shuleni pamoja na uhamasishaji wa wananchi kuzingatia lishe bora hasa katika vituo vya kutolea huduma ya afya na katika jamii.
Ndugu Kitungi amewasisitiza wataalam kuendelea kutoa elimu ya lishe bora katika jamii pamoja na kuwahimiza wananchi wa Mafia kulima mbogamboga na kupanda miti ya matunda kwa wingi.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.