Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Pwani, leo Machi 18, 2025 imefanya ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyopo wilayani Mafia kwa lengo la kufuatilia hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na mradi wa maji wa Kifinge katika kata ya Baleni, zahanati ya kijiji cha Kibada iliyopo kata ya Baleni na mradi wa barabara ya Kichangachui-Msufini katika kata ya Kilindoni.
Ziara hiyo ilitanguliwa na ziara ya timu ya wataalam ya mkoa wa pwani ilyofanyika Machi 17, 2025 ikiambatana na kamati ya usalama ya wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Mangosongo pamoja na timu ya wataalam wa Halmashauri.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.