Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ( MSLAC) imeanza rasmi kutekelezwa wilayani Mafia ikihusisha wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, wataalam wa Halmashauri wakiwemo Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Sheria, Ustawi wa Jamii na taasisi binafsi pamoja na wadau katika kutoa elimu.
Utoaji wa elimu wa Kampeni hiyo umejikita katika kujenga uelewa wa masuala ya migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, ukatili wa kijinsia, matunzo kwa watoto pamoja na ajira.
Kampeni hii ni mahsusi kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ambao wanapata changamoto ya namna ya kuifikia huduma ya kisheria kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha pamoja na kukosa elimu ya kutosha katika masuala mbalimbali.
Wananchi 515 katika makundi mbalimbali ya kijamii wamefikiwa, ambapo Februari 25, 2025 huduma ilitolewa katika kata ya ndagoni na inatarajiwa kuendelea leo Februari 26, 2025 katika vijiji vya Kanga na Bweni.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.