Kampeni ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira ijulikanayo kama " Soma na Mti" imezinduliwa wilayani Mafia ikitarajiwa kutekelezwa katika Shule za Msingi na Sekondari.
Kampeni hiyo inayosimamiwa na wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ina lengo kubwa la kukabiliana na uharibifu wa mazingira ambao husababishwa na shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akipokea kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mwl. Kassim Ndumbo amewahakikishia wataalam hao kuwa Halmashauri ipo tayari kufanya nao kazi kwa ukaribu ili kuleta elimu na hamasa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
" Tunaendelea kuhamasisha jamii kupanda miti, ingawa kwa kiasi fulani jamii bado inakuwa kikwazo, hasa linapokuja suala la kuitunza miti iliyopandwa" alisema Mwl. Ndumbo.
Kampeni ya " Soma na Mti" inaendeshwa nchi nzima na imeanza kwa hatua ya kupanda miti 81 kwa shule tano wilayani Mafia ambazo ni Shule za Sekondari za Kilindoni, Kitomondo na Rhapta pamoja na Shule za Msingi za Sikula na Mrambani.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.