Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) chini ya mchungaji Nehemia Mosha limetoa msaada wa box 2 za pamba za wakina mama, vibana vitovu (cord clamp -100 kwa watoto wanaozaliwa) , box 1 moja la gloves( 100 PC's) na mabenchi 6 ya kukalia kwa ajili ya wagonjwa. Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Kassim S. Ndumbo katika hospitali ya Wilaya leo tarehe 03/11/2022.
Mkurugenzi amemshukuru Mchungaji Mosha kwa kuwa na moyo wa kusaidia wagonjwa kwani imekuwa desturi yake kutoa sadaka katika hospitali hiyo.
Akitoa shukrani Mganga Mkuu (W) Dr. Zuberi Mzige amesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia wakina mama na watoto ambao hawana uwezo, na mabenchi yatapelekwa katika zahanati mpya za Kifinge na Gonge
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.