Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) Bw. Zurab Pololikashvili ameahidi kutembelea kisiwa cha Mafia wakati wa Jukwaa la pili la Kimataifa la Utalii wa vyakula linalotarajia kufanyika kuanzia Tarehe 23 mpaka 25 Aprili 2025, ambapo Tanzania ni Mwenyeji wa Mkutano huo Kikanda.
Hilo limewekwa wazi wakati Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ikiendelea kuipaisha Mafia Kimataifa kwa kuitangaza katika majukwaa mbalimbali ambapo Machi 06, 2025 Tanzania ilipata nafasi ya kujitangaza kiutalii katika maonesho makubwa ya Utalii Duniani ya ITB yanayofanyika nchini Ujerumani, Berlin huku Kisiwa cha Mafia kukiwa miongoni mwa maeneo yaliyotangazwa kwa kuwa na vivutio vizuri na vya kipekee kwa utalii.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.