Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Ndugu Shabani Shabani amewataka walimu kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia miongozo iliyopo katika taaluma yao ili kuboresha elimu wilayani na Taifa kwa ujumla.
Ndugu Shabani ameyasema hayo leo Oktoba 2, 2025 wakati wa kikao na walimu wa shule ya msingi ikiwa ni siku ya pili ya kukutana na walimu wa shule zote za msingi na sekondari kwa lengo la kusikiliza kero pamoja na kuwakumbusha masuala ya msingi katika majukumu yao.


Ameeleza kuwa, ni muhimu kwa walimu kufanya kazi kwa kuzingatia mambo matatu makubwa ambayo ni sheria, kanuni na taratibu za kazi, nidhamu pamoja na kuipenda kazi yao ili kuleta matokeo chanya." Kuwa mwalimu ni zaidi ya kufundisha darasani, nje ya kazi pia ni muhimu kwa mwalimu kuishi kwa kuonesha mfano mzuri kwa jamii, maana hata mwanafunzi anaweza kuiga mazuri kutoka kwa mwalimu wake. Mambo haya matatu si kwa walimu tu pekee, ila watumishi wote ni muhimu kuzingatia haya" alieleza.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kujizatiti katika kuhakikisha inaboresha elimu pamoja na mazingira ya kazi ikiwemo kulipa stahiki zao, kuajiri walimu wapya pamoja na kuboresha miundombinu.


Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.