Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bi. Zuwena Omary Jiri katika ziara aliyofanya wilayani ya Mafia amekutana na watumishi na idara na sekta mbalimbali za serikali sikunl ya tarehe 04/11/2022 ukumbi wa mkuu wa wilaya alieesema amekuja kwa lengo kupafahamu Mafia, kujua fursa na changamoto zake, na zaidi kushukuru na kuwapongeza kwa kuendelea kulitumikia taifa kijasiri
Alisema "serikali ni mtumishi wa umma kuanzia ngazi ya chini kabisa , na usifikiri kuwa kuna serikali sehemu nyingine , tuonyeshe ukubwa, uzuri na uimara wa serikali"
Alisisitiza kufanya kazi kwa bidii na maarifa na sio kufanya kazi kwa mazoea, kuacha mawazo ya kuhama kwani "tunahitajika kukua kiutumishi na tusiwaze kuletwa mafia ni kama adhabu"
Pia alitoa fursa kwa watumishi ambapo Afisa Utumishi (W) alisema halmashauri ina uhaba wa watumishi na watumishi wanaoletwa ni wachache kulingana na ikama aliongeza kwa kusema changamoto zilizochangia watumishi wasiripoti ama kuomba kuhama ilichangiwa na hali ya usafiri ambayo kwa sasa kwa sasa imepata tiba
Naye Afisa Kilimo alishauri kuendelea kuomba kuletewa watumishi na pia watumishi wapewe motisha mwisho alishauri kuwe na uhamisho wa ndani ya mkoa angalau ndani ya miaka 03-05 ifanyike mzunguko ( rotation)
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.