Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ally ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa usimamizi mzuri wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ambao umekuwa ukiwainua wajasiriamali hasa katika shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Ally ametoa pongezi hizo leo Agosti 4, 2025 alipotembelea banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Mafia katika maonesho ya nanenane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Ametoa wito kwa wajasiriamali kuitumia fursa ya mikopo hiyo inayotolewa na Serikali ili waweze kukuza mitaji yao na kuboresha biashara zao katika kutafuta masoko na kuongeza thamani za bidhaa wanazozalisha.
Katika hatua nyingine, amewataka wataalam na viongozi wilayani Mafia kuendelea kutoa elimu juu ya uwepo wa mikopo hiyo pamoja na taratibu za msingi za kuwezeshwa mikopo hiyo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia Ndugu. Shabani Shabani ememshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka sera bora zinazotoa fursa kwa wananchi kujiendeleza kiuchumi, hasa katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Kilindoni-Bomani Street
Anuani ya posta: 85
Simu: 0232010199
Simu ya mkononi:
Baruapepe: ded.mafia@pwani.go.tz / ded@mafiadc.go.tz
Copyright ©2017 Mafia District Council . All rights reserved.